Sambaza

KICHANGA ALIYEKAA TUMBONI WIKI 21 TU

TAARIFA ikufikie kwamba kichanga aliyezaliwa katika wiki ya 21 huku akiwa na uzito wa 420g nchini Marekani, amevunja rekodi ya dunia ya kuwa kichanga aliyezaliwa kabla ya muda wake lakini akapata bahati ya kuendelea kuishi.

Madaktari wameeleza kuwa ni nadra mno kwa kichanga anayezaliwa katika wiki ya 21 kuendelea kuishi, mama wa kichanga hicho alikimbizwa hospitali Julai 4, 2020 ambapo alijifungua watoto wawili Curtis na C’Asya  isivyo bahati dakika chache baada ya kujifungua, C’Asya alifariki dunia huku akimuacha Curtis ambaye alikuwa kwenye hali mbaya.

Curtis aliwekwa kwenye uangalizi mkubwa wa madaktari bingwa huku akiwa kwenye mashine maalumu ya ‘Ventilator’ ambapo alidumu kwa siku 275 hospitalini na baadaye kuruhusiwa. Guinness World Record imethibitisha kuwa mtoto huyo kwa sasa ana miezi 16 na afya yake ni njema, na hivyo kuweka rekodi ya dunia ya kuwa kichanga aliyezaliwa kabla ya muda na kupata nafasi ya kuendelea kuishi.

Cc; @bakarimahundu        

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey