Sambaza

Kundi la BTS Lililotikisa MTV Ema

Kundi la muziki wa pop la BTS kutokea nchini Korea Kusini limeshangaza dunia baada ya kunyakua Tuzo 4 za MTV EMA katika vipengele vya; Best Pop, Best K-pop, Best Group na Biggest Fans, ugawaji wa tuzo hizo ulifanyika Novemba 14, katika ukumbi wa Budapest Sports Arena, nchini Hungary.

Kundi la BTS lilianza kufahamika rasmi mwaka 2013, likiwa limeundwa na wasanii 7 ambao ni; Jin, Suga, J-Hope, RM, Jimin, V na Jungkoo ambao wote ni raia wa nchi ya Korea Kusini.

Albamu yao ya ‘Love Yourself: Answer’ ilitikisa hadi mitandao mikubwa kama Billboard na kupelekea Rais wa nchi ya Korea Kusini Moon Jae-in kuwapongeza vijana hao kupitia mtandao wa Twitter, pia wamewahi kushika nafasi ya kwanza kwenye mtandao wa iTunes katika nchi 91 duniani kupitia albamu yao ya Map of The Soul: 7, huku upande wa YouTube wakiwa na wafuatiliaji ‘Subscribers’ 60.7M.

BTS mwaka 2018 walikuwa ni wasanii wa kwanza kutoka Korea kualikwa kuhutubia kwenye mkutano wa umoja wa mataifa (UN) mbele ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres pamoja na Rais wa Korea Kusini Moon Jae-in.

Cc; @bakarimahundu

 

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey