PWEZA, KAA NA KAMBA KUTUNGIWA SHERIA
Serikali ya Uingereza imetaka viumbe jamii ya Pweza, Kaa na Kamba kutambuliwa na kupewa ulinzi chini ya sheria mpya ya ustawi wa wanyama kutokana na viumbe hao kuwa na uwezo wa kupata mateso na maumivu kutokana na hisia kali walizonazo.
Ripoti ya tafiti 300 za kisayansi imethibitisha kuwa viumbe jamii ya Pweza, Kamba na Kaa wanahisia kama ilivyo kwa viumbe hai wengine, hivyo kuwaweka viumbe hao katika kundi la viumbe wenye hisia.
Ripoti hiyo imependekeza kuwa viumbe jamii ya kaa na Pweza hawapaswi kuchemshwa wakiwa hai, pia kuwekewa taratibu mzuri za uchinjaji na usafirishaji.
Cc; @bakarimahundu
Toa Maoni Yako Hapa