RIHANNA SHUJAA WA TAIFA BARBADOS
Hii ni habari njema kwa mashabiki wa mwanamuziki na mshindi wa Grammy Rihanna, ambapo Waziri Mkuu, Mia Mottley kwa niaba ya Serikali ya Nchini Barbados amemtangaza Rihanna kuwa shujaa wa taifa hilo.
Rihanna ametangazwa kuwa shujaa wa taifa wakati wa sherehe za taifa hilo kuwa Jamuhuri zilizofanyika katika mji mkuu wa Bridgetown nchini humo, sherehe hizo ziliuzuliwa na watu maarufu duniani kama Price Charles na mchezaji kriketi Sir Garfield, Rihanna alipokea heshima hiyo mbele ya Rais mpya wa taifa hilo, Dame Sandra Mason.
Cc; @bakarimahundu
Toa Maoni Yako Hapa