Sambaza

Familia Yakataa Ofa Ya Travis Scott

Familia ya mtoto mdogo wa miaka 9 aliyefariki kwenye tamasha la Travis Scott linalojulikana kama Astroworld, imekataa ofa ya msanii huyo ya kugharamia mazishi pamoja na kukutana ana kwa ana na familia.

Mtoto huyo anayejulikana kama Ezra Blount, alikutwa na mauti wakati wa vurugu zilizoanza wakati rapa Travis Scott alipopanda jukwaani, vyanzo vya habari vinaeleza kuwa Travis Scott alitoa ofa ya kugharamia mazishi pamoja na kuomba kukutana na wanafamilia wa mtoto huyo.

Taarifa za kukataliwa kwa ofa hiyo imethibitishwa na mwanasheria wa familia ya mtoto huyo.

Cc; @bakarimahundu

 

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey