Sambaza

Rihanna Adaiwa Kuwa Mjamzito Kwa Mara Ya Kwanza

Tetesi zilizoanza mwezi Septemba mwala 2021, zikimuhusisha mwanamuziki tajiri na shujaa wa taifa la Barbados kuwa na ujauzito zimeanza kuwa ni ukweli baada ya staa huyo kuonekana akiwa na tumbo linaloashiria uwepo wa ujauzito huo.

Vyombo mbalimbali vya habari duniani vimeripoti taarifa hiyo baada ya Rihanna kuonekana katika hafla ya kusherehekea Jamuhuri ya Barbados iliyofanyika wiki hii katika mji wa Bridgetown, Rihanna alionekana huku akiwa anaficha ficha tumbo lake ambalo linaashiria kuwa ana ujauzito.

Taarifa za ujauzito wa Rihanna zimethibitishwa na rafiki wa kalibu wa staa huyo ambaye alimsindikiza kupanda ndege binafsi, huku mpenzi wake wa muda mrefu ASAP Rocky akihusishwa moja kwa moja na ujauzito huo. Huu ni ujauzito wa kwanza kwa Rihanna na Kama atafanikiwa kujifugua basi atakuwa ni mtoto wa kwanza kwa staa huyo.

Cc; @bakarimahundu

 

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey