TREY SONGZ AHUSISHWA UNYANYASAJI WA KIJINSIA
Muimbaji na Muigizaji Tremaine Aldon Neverson, almaarufu Trey Songz amejikuta akihusishwa kwenye tuhuma nzito za unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya mwanamke mmoja aliyeripoti tuhuma hizo katika kituo cha polisi cha Las Vegas, Nevada nchini Marekani.
Mwanamke huyo anamtuhumu Trey Songz kwa kumfanyia unyanyasaji wa kijinsia katika hotel moja iliyopo Las Vegas, kwa mujibu wa ripoti za kipolisi zimeonesha kupokelewa kwa tuhuma hizo lakini hakuna zoezi lolote la ukamataji lililofanyika. Hili siyo jambo geni kwa Trey Songz kwani mwaka 2020, mwanamke aliyefahamika kwa jina la Aliza alimtuhumu Trey kumfanyia vitendo vya unyanyasaji ikiwemo kumzuia kutoka katika chumba walichokuwepo na kumkojolea mkojo katika mwili wake.
Polisi wa Las Vegas wamethibitisha kushirikiana na msanii Trey Songz katika upepelezi wa kesi hiyo, hadi sasa Trey hajalizungumzia tukio hilo sehemu yoyote.
Cc; @bakarimahundu