WILL SMITH: NATAPIKA NIKIFIKA KILELENI
Muigizaji na mwandishi wa kitabu cha ‘WILL’, Will Smith ameweka wazi namna alivyosalitiwa na mpenzi wake akiwa na umri wa miaka 16 hadi kufikia hatua ya kufanya mapenzi na wanawake wengi ambapo kila alipokuwa akifika kileleni basi alikuwa anatapika.
Katika kitabu hicho cha ‘WILL’ , Will Smith amefunguka jinsi alivyojikuta kwenye urahibu wa ngono baada ya kusalitiwa na mpenzi wake aliyemtaja kwa jina la Melanie Parker,wawili hao walikutana shuleni na hapo ndipo mapenzi yalipoanzia. Ndani ya kitabu hicho Smith amefunguka mengi juu ya kumbukumbu za maisha yake ikiwemo kukutwa na mama yake mzazi akifanya mapenzi jikoni na mpenzi wake huyo wa zamani.
Wawili hao waliendelea kuwa kwenye mahusiano baada ya tukio hilo, lakini waliachana pale Smith alipogundua kuwa msichana huyo amemsaliti, na hapo ndipo Smith alipoingia kwenye uraibu wa ngono. Smith amebarikiwa kupata watoto watatu, Trey (29) aliyezaa na Zampino na Jaden (23) na Willow (21) aliozaa na mwanamama Pinkett Smith.
Cc; @bakarimahundu