Sambaza

AMSHITAKI DAKTARI KWA KURUHUSU AZALIWE

Mwanamke mmoja anayejulikana kama, Evie Toombes (20)  kutokea Uingereza, atalipwa mabilioni ya pesa baada ya kushinda kesi aliyoifungua dhidi ya Daktari Philip Mitchell aliyemzalisha mama yake, kwa kuruhusu yeye kuzaliwa wakati daktari huyo alijua kuwa angezaliwa na ugonjwa wa uti wa mgongo ‘Spina Bifida’.

Ugonjwa huo wa uti wa mgongo unamfanya Evie ashinde saa 24 kwa kutumia mirija maalumu ili aweze kuendelea kuishi,Eve amemfikisha Dkt Philip mahakamani kwa kile alichokiita ni kosa alilolifanya daktari huyo la kutokumshauri mama yake juu ya mimba aliyoibeba ili aweze kuitoa na yeye asizaliwe.

Jaji wa kesi hiyo, Rosalind amemuunga mkono Eve na kutaka alipwe kiasi cha pesa ili kufidia mateso anayoyapata  kutokana na ugonjwa huo, huku mwanasheria wa Eve akithibitisha taarifa hizo kwa  kuweka wazi kuwa Eve atalipwa mabilioni ya pesa ili kufidia mateso ya ugonjwa huo tangu utoto wake hadi mwisho wake wa maisha.

Cc; @bakarimahundu

 

 

 

 

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey