Sambaza

‘THE ROCK’, BTS WAKIMBIZA TUZO ZA PEOPLE’S CHOICE

Washindi wa Tuzo za People’s Choice kwa mwaka 2021, wametangazwa katika usiku wa ugawaji wa tuzo hizo uliofanyika Desemba 7,2021 katika Ukumbi wa Barker Hangar Santa Monica, uliopo California nchini Marekani ambapo jumla ya vipengele 40 vilikuwa vinashindaniwa.

Mwigizaji Dwayne Johnson maarufu kama ‘The Rock’ ameng’ara zaidi kwenye tuzo hizo upande wa waigizaji wa kiume ambapo amejizolea tuzo tatu katika vipengele vya; Muigizaji Bora wa Kiume, Muigizaji Bora wa Filamu za Vichekesho kupitia filamu yake ya Jungle Cruise ambapo pia ametunukiwa Tuzo ya Heshima.

Kundi la Muziki la BTS kutoka Korea Kusini, kwa mara nyingine limeng’ara kwenye tuzo hizo na kunyakua tatu kwa mpigo, huku mwanadada staa wa Hollywood, Scarlet Johansson akinyakua tuzo mbili.

Kwa upande mwingine, Filamu ya Kikorea ya Squid Game nayo imeng’ara kwa kupata tuzo katika kipengele cha filamu iliyotazamwa na watu wengi zaidi

Cc; @bakarimahundu

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey