Sambaza

JAY-Z ANUNUA SAA YA BIL. 14

Rapa wa kiwango cha dunia kutoka nchini Marekani ambaye ni Mshindi wa wakati wote wa Tuzo za Grammy na mfanyabiashara mkubwa, Jay-Z anakuwa mtu wa kwanza kumiliki saa aina ya Tiffany & Co X Patek Philippe, yenye thamani ya Dola za Kimarekani milioni 6.5 (zaidi ya shilingi bilioni 14 za Kitanzania), ikiwa ni siku chache tu tangu kuachiwa rasmi kwa toleo la saa hizo sokoni.

Saa hizo zimetengenezwa kufuatia muungano wa Kampuni ya Tiffany & Co na ile ya Patek Philippe, katika kusherehekea miaka 170 ya Kampuni ya Patek Philippe.

Desemba 11, 2021 saa hizo ziliingia rasmi sokoni, zikiwa jumla ya saa 170 tu huku Jay-Z akiwa ni mtu wa kwanza kuonekana amevaa mapema wiki hii.

Cc; @bakarimahundu

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey