KANYE KUGEUZA MIJENGO YAKE KUWA MAKANISA
Rapa Kanye West, amesema hatokuwa na makazi kwa mwaka mmoja, kwa kubadilisha mijengo yake ya thamani kuwa makanisa na mingine kuwa vituo vya watu wasiokuwa na makazi ambapo chakula kitapatikana muda wote.
Katika mahojiano aliyoyafanya na Jarida la 032c, Kanye West amesema atafanya hivyo baada ya kupata sehemu ya mali zake katika mgao na mtalaka wake, Kim Kardashian.
Haya yanakuja siku chache baada ya mtalaka wake, Kim Kardashian kutangaza kuondoa jina la West katika bidhaa zake za urembo.
Cc; @bakarimahundu
Toa Maoni Yako Hapa