Sambaza

50 CENT ATANGAZA KUACHA MUZIKI

Rapa mkongwe na mwigizaji wa nchini Marekani, 50 Cent kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram  ameweka wazi nia yake ya kuachia albamu Desemba mwaka huu, ambayo huenda ikawa ndiyo kazi yake ya mwisho kwenye soko la muziki.

Hii siyo mara ya kwanza kwa 50 Cent kutangaza kustaafu muziki kwani amekuwa akitangaza kustaafu muziki kwa miaka kadhaa, mwaka 2016, 50 Cent alitangaza kuacha muziki baada ya kutoa albamu yake ya ‘Street King Immortal’.

Katika ukurasa wake wa mtandao wa Instagram, 50 Cent aliandika ‘‘Albamu yangu inayofuata inaweza kuwa ni ya mwisho’’ ( my next album might be my last).

Cc; @bakarimahundu

 

 

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey