Kenya: Jaguar Afikishwa Mahakamani, Anyimwa Dhamana
MBUNGE wa Jimbo la Starehe nchini Kenya, Charles Jaguar, amefikishwa mahamani kwa tuhuma za uchochezi.
Jaguar ambaye pia ni mwanamuziki wa miondoko ya ‘hip pop’, alifikishwa mahakamani leo Alhamisi June 27, baada ya kulala polisi kwa siku moja.
Jana mbunge huyo alikamatwa na jeshi la polisi akiwa katika viwanja vya bunge alipokuwa akihudhuria vikao vya bunge la bajeti.
Baadaye jioni Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) kupitia ukurasa wake wa Twitter iliandika: “Jaguar anazuiliwa kwa tuhuma za kutoa matamshi ya chuki, uchochezi na kuvuruga amani.”
Jumatatu iliyopita mbunge huyo alionekana katika video fupi ambayo ilisambaa katika mitandao ya kijamii akizungumza na wafanyabiashara wa jijini humo na kuwaeleza kuwa hawatokubali watu wa nje waje kufanya biashara nchini mwao.
”Wakenya ni sharti wafanye biashara zao bila kushindana na watu kutoka mataifa mengine. Raia wa Pakistan wametawala biashara za kuuza magari nchini humu, Watanzania na Waganda wanatawala katika masoko yetu. Tunasema imetosha iwapo hawatarajeshwa nyumbani katika saa 24 tutawashika na kuwapiga na hatuogopi mtu yeyote,” alisisitiza mbunge huyo.
Duh! ZITTO ACHARUKA BUNGENI – “Tunaiua Tanzania, Ongozeni Sio Kutawala”