Sambaza

Hatua 4 Za Ndoa Yao, Diamond naTanasha Watikisa Afrika nzima

STAA wa Bongo Fleva anayefanya freshi Afrika, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na mchumba wake, Tanasha Donna Oketch wameshaanza kutikisa katika safari yao ya kuelekea kufunga ndoa kama ambavyo wenyewe wameitangazia dunia. 

Awali, Tanasha na Diamond walitarajiwa kufunga ndoa Siku ya Wapendao ‘Valentines Day’, Februari 14, mwaka huu huku ikitangazwa kuwa wangehudhuria mastaa wakubwa akiwemo mwanamuziki wa Marekani, William Leonard Roberts ‘Rick Ross’, lakini ghafla tukaambiwa mambo yamekwama, tutatangaziwa upya.

Hata hivyo, Diamond juzikati aliwaambia waandishi wa habari kuwa, Julai 7, mwaka huu atafanya tukio kubwa litakalotikisa ambapo mpango mzima utakuwa ni ndani ya Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar

Akijibu swali la mwandishi wa habari kuhusu lini atamuoa rasmi Tanasha baada ya kuahirisha kwa muda mrefu, Diamond alisema watu wasubiri kwani tarehe aliyoitaja ulimwengu utashuhudia tukio kubwa.

Alipoulizwa kama ndiyo siku ya kufunga ndoa au kumvisha pete ya uchumba Tanasha kama ambavyo imekuwa ikienezwa, Diamond alisema; “Ninyi subirini mtaona.”

MBWEMBWE ZAANZA KUTIKISA

Siku chache baada ya Diamond au Mondi kueleza kuwa kuna tukio kubwa linakuja, wikiendi iliyopita zilianza kusambaa video na picha zikiwaonesha yeye na Tanasha wakiwa wamevalia mavazi rasmi ya kisherehe huku wakicheza muziki.

Katika video hizo pia wanaonekana mama Diamond, Sanura Kassim ‘Sandra’ na mumewe Maisara Shamte wakicheza kwa furaha bila kujulikana ilikuwa ni katika tukio gani.

TETESI ZA KUVISHANA PETE

Baada ya video na picha hizo kuvuja, kwenye mitandao mbalimbali ya ndani na nje ya Bongo ishu ya kwamba wawili hao wameshaanza safari ya kuelekea kwenye ndoa ilitikisa ambapo mitandao ya habari za burudani ya Nigeria, Kenya, Sauzi na kwingineko iliripoti kuhusu tukio hilo.

“Kwa hatua hii ya kwanza inaonekana itakuwa shughuli kubwa, tusubiri tuone maana wengi wanatamani kuona ndoa itakuwa ya aina gani,” uliandika mtandao mmoja wa habari za mastaa nchini Nigeria. Mtandao mwingine wa Kenya uliposti picha ya Diamond na Tanasha wakicheza kisha kuonesha kutoelewa kilichokuwa kikiendelea kutokana na muonekana wa wachumba hao; “Hii ni nini? Ndoa au ‘ingejimenti’?”

Wakati picha na video hizo vikitikisa bila kujulikana ni nini, mmoja wa watu wa karibu wa Diamond aliandika kwenye ukurasa wake wa Instagram kuwa, video hizo ni maandalizi ya kupiga picha za promo. “Maandalizi ya picha za promo……..! Naambiwa tarehe 7, Mama Dangote (Mama Diamond) anataka kulisimamisha jiji pale Mlimani City ila wamependeza, itakuwa wameshona Mobeto Styles.”

Maelezo hayo yalionesha kuwa, tukio hilo halikuwa la kuvishana pete wala ndoa bali ilikuwa ni maandalizi tu ya kupiga picha za promo kuhusu eventi itakayofanyika Julai 7.

Kufuatia udambwidambwi huo, baadhi ya wadau walikomenti wakisema kuwa, kama ni maandalizi ya picha tu za promo ya tukio, je, tukio lenyewe litakuwaje?

“Yaani kuelekea kwenye kufunga ndoa, tutaona mbwembwe nyingi sana, hapa ni fujo za maandalizi ya picha tu za hilo tukio la keshokutwa, sasa hatua ya pili ya kuvishana pete, hatua ya tatu ya send off… ya nne ya kufunga ndoa, sijui mambo yatakuwaje, sisi yetu ni macho na masikio tu…” Aliandika mdau mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Sandry.

Mbali na amshaamsha iliyopo kwenye mitandao ya kijamii na tovuti mbalimbali Afrika, wapo ambao wametoa tahadhari kuwa safari hii wanataka kuona mambo yanatokea na kwamba mbwembwe hizo zikiishia njiani, watawapuuza mpaka watakoma.

“Natamani kuona ndoa inafungwa, yasije kutokea yale ya Zari maana kipindi kile tuliona Diamond na Zari walitupia picha kama hizihizi na wakadai eti wamefunga ndoa, lakini kumbe ilikuwa geresha, sasa ikiwa hivyo kwa Tanasha, tutaona kwamba wanachukulia sisi mapoyoyo, nitawachukia sana…”

Aliandika huko Insta shabiki mmoja chini ya video inayowaonesha wachumba hao wakicheza muziki.

ZARI AFUNGUA MDOMO

Wakati vurugu hizo zikiendelea kutikisa, Zari naye hakukaa kimya bali kupitia Insta Live alionekana akijinadi kuwa naye anatarajia kufunga ndoa Siku ya Mandela ‘Mandela Day’, Julai 18, mwaka huu huku akieleza kuwa, anaamini siku hiyo itakuwa ni furaha kwake na itatikisa Afrika.

“Rasmi nitaolewa Siku ya Nelson Mandela, itakuwa ni kitu kizuri sana na naamini Afrika itaona,” alisema Zari.

Pakua App ya +255 Global Radio ili Kusikiliza Vipindi vyetuBofya HAPA KUINSTALL APP

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey