Sambaza

Rais Ajiuzulu, Kocha wa Misri Atimuliwa baada ya Kutolewa AFCON

Kocha Mkuu wa timu ya soka ya Taifa Misri, Javier Aguirre (60) ametimuliwa baada ya ‘The Pharaohs’ kutolewa kwenye michuano ya Kombe la Mataifa Afrika (Afcon) kwa kufungwa bao 1-0 na timu ya Afrika Kusini.

Baada ya mchezo wa jana jijini Cairo, kocha huyo raia wa Mexico alisema anastahili lawama kwa kuondolewa kwenye michuano hiyo na kwamba, leo angejadiliana na Chama Cha Soka Misri (EFA) kuhusu hatma yake.

Muda mfupi baada ya kocha huyo kutimuliwa, Rais wa EFA Hany Abou-Rida nae alitangaza kujiuzulu na akawataka wasaidizi wake waandike barua za kuachia ngazi.

Aguirre alianza kuifundisha timu hiyo Agosti mwaka jana, na tangu wakati huo ‘The Pharaohs’ wamecheza mechi 12, wameshinda tisa, wametoka sare moja, wamefungwa mechi 2 ikiwemo ya jana.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey