Sambaza

Msanii Ziggy Wine wa Uganda, Auawa Kikatili

Mwanamuziki wa nchini Uganda, Ziggy Wine ambaye alikuwa chini ya usimamizi wa ‘Lebo’  ya mwanamuziki/mwanasiasa  Bobi Wine amefariki dunia usiku wa jumapili tarehe 4, Augusti 2019.

Ziggy Wine ambaye jina lake halisi ni Michael Kalinda amefariki baada ya kutekwa tarehe 21 July na kupigwa vibaya alipokuwa  njiani akielekea studio za Firebase Crew, inaelezwa kuwa baada ya watekaji kukamilisha unyama huo walimtupa pembezoni mwa hospitali ya Mulago iliyopo Jijini Kampala ambapo alikutwa akiwa amejeruhiwa vibaya huku jicho lake la kushoto likiwa limetobolewa, vidole vyake vya mkononi vikiwa vimekatwa.

 

Bobi Wine, mbunge wa Kyadondo Mashariki  ambaye pia alikuwa akimsimamia Ziggy kimuziki tayari ameshazungumzia suala hilo, kupitia ukurasa wake wa twitter Bobi Wine ameandika ;

“Ziggy alipatikana akiwa amejeruhiwa vibaya kwa kupigwa na kuteswa, jicho lake moja la kushoto likiwa limetolewa na vidole vyake viwili vikiwa vimekatwa, na zaidi ya hapo wamemuibia kila kitu alichokuwa nacho na kisha kumtupa pembeni ya hospitali ya Mulago”.

Vyanzo vya habari nchini Uganda vimeliambia gazeti la Daily monitor  la nchini humo kuwa baada ya kutekwa na kujeruhiwa vibaya, Ziggy alilazwa katika Hospitali ya Mulago kwa zaidi ya wiki moja katika kitengo cha wagonjwa mahututi lakini hakupatiwa matibabu yoyote yanayostahili kwa makusudi, kitendo kilichofanya familia yake kulalamikia uongozi wa hospitali hiyo.

Ripoti kutoka hospitali ya Mulago inaeleza kuwa, Ziggy amefariki baada ya kujeruhiwa vibaya sehemu ya ubongo wake, na kuwa uchunguzi wa CT Scan ulibaini kuwa kuna damu nyingi ilivujia ndani ya ubongo.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey