Inauma sana! Vuta picha kama mzazi, umekwenda kwenye mihangaiko yako, unarudi unaambiwa watoto wako wanne wamefariki dunia ghafla, hakika inasikitisha!
Hali hiyo ndiyo imetokea kwenye familia ya Said Saleh, mkazi wa Majaribio, Tandika jijini Dar, ambaye Tarehe 15 Disemba ilikuwa nzito kwake kufuatia kupewa taarifa za wanawe watatu wa kuwazaa, Jalila (16 ), Khalfan (14 ) Ruuman (15) ambao ni watoto wa familia moja pamoja na Mariam Said Ramadhani ambaye ni ndugu wa familia hiyo, walifariki kwa wakati mmoja.