HIT MAKER wa ngoma ya UNO, Harmonize au Konde Boy amefanya shoo ya aina yake iliyoandika historia kwa mara ya kwanza akipanda na kufanya shoo kubwa kwenye Jukwaa la Fiesta usiku wa kuamkia leo, Jumatatu, desemba 9, 2019. Tamasha hilo ambalo ni kilele chake kimefanyika katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam limehudhuriwa na amelfu ya mashabiki huku wasanii zaidi ya 38 wakipata fursa ya kupanda jukwaa na na kuwapa burudani mashabiki wao.