MSEMAJI wa Klabu ya Simba Haji Manara akiwa na Mtendaji Mkuu wa Simba, Senzo Mazingisa leo Januari 1, 2019 wameongea na wanahabari katika hoteli ya Serena kuongelea mchezo wa Simba SC dhidi ya Yanga SC utakaochezwa siku ya Jumamosi saa 11: 00 jioni Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Haji Manara amesema Yanga ni Timu kubwa na kuwataka wachezaji wasiwe na mapembe badala yake wajiandae vyema, wakapambane.