Giza limeendelea kutanda kufuatia mbwa 300na paka kadhaa kukutwa hivi karibuni Ndani ya nyumba ya serikali Oysterbay Mtaa wa Mawenzi Kitalu Namba 823, Jijini Dar es salaam.
Habari hiyo ilienea kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii Bado imeacha sintofahamu na maswali mengi juu ya matumizi ya Wanyama hao.
Watu wengi kwenye mitandao ya kijamii wamekuwa wakijadiliana ni vipi nyumba hiyo ya serikali ya kisasa iliweza kuhifadhi wanyama hao bila kujulikana matumizi yake.