Marioo Anavyoitawala Chati Ya Ngoma Kali Wiki Hii
Kwa mujibu wa Application ya Boomplay, Marioo ni mwanamuziki anayesikilizwa mara nyingi kwenye nafasi za juu wiki hii.
Ngoma zake mbili alizoachia siku za hivi karibuni zote zinafanya vizuri. Wakati ambao Anyinya inapambana kutafuta nafasi ya pili kwenye chati ya nyimbo 100 zinazosikilizwa Tanzania, Ngoma yake nyingine Ya Uchungu ipo nafai ya 5 ikionyesha ishara zote za Marioo kusogea nafasi ya juu zaidi.
Baada ya kumcheki Marioo na kumuuliza kuhusu ishu hii, alionekana kuwa so excited kwa kusema hachukulii poa kwani hiki ni kitu kikubwa sana. Kuingiza nyimbo mbili kwenye nafasi tano za juu kati ya nyimbo 100 zinazosikilizwa wiki nzima sio kitu kidogo.
Chati hiyo ambayo ilichapishwa Jumatano (Oktoba 9), imepambwa na ngoma kali kama Yope ya Innos’b na Tanzanian supastaa Diamond Platnumz ambayo ipo kwenye nafasi ya kwanza kila kona. Kolabo ya Roma na Stamina (ROSTAM) na Nay wa Mitego ‘Kijiwe Nongwa’ ipo kwenye nafasi ya pili huku nyimbo mbili za Marioo zikiwa zimeiweka katikati Kiza Kinene ya Nandy, Nafasi ya ya sita inamilikiwa na mkali wa Nigeria Mr P, aliyekuwa anaunda kundi la P Square na ngoma yake Karma. Naenjoy ya Aslay ipo nafasi ya 7 kati ya ngoma 100 zinazosikilizwa Bongo wiki hii akifuatiwa na EX- Memba wake wa Yamoto Band, Mboso ambaye anatamba kwenye nafasi ya 8 na shilingi aliyomshirikisha Reekado Banks wa Nigeria.
Top 10 ya ngoma kubwa Bongo, inaendelezwa na The Finnest Of Arusha, Gnako WaraWara na Maua Sama kwenye mkwaju wao Gusanisha ambao upo nafasi ya tisa unaoungana na shilingi ya Mbosso pamoja na Naenjoy ya Aslay kama ngoma ambazo zinashuka kwenye chati, huenda zikapotea soon.
Ngoma inayokamilisha Top 10 ya chati hii ni Bugana ambayo ni kolabo ya Billnass na Nandy anayefanya poa na Kiza Kinene aliyowashirikisha sauti Sol ambayo ipo nafasi ya nne.
Kuhusu kumiliki chati ya Top 5, Marioo haijaishia hapo tu, bado ameendelea kusikilizwa kwenye nyimbo 20 bora kwenye ngoma kama Raha inayoporomoka kutoka nafasi ya 13 na Inatosha ambayo inapanda kutoka nafasi ya 18 kwenda 17 zote zikimuweka TOTO BAD kwenye nafasi ya msanii mwenye ngoma nyingi kati ya ngoma 20 akiwa na ngoma nne, anafuatiwa na Diamond Platnumz mwenye ngoma 3.
4,816 total views, 3 views today