Sambaza

Msanii Kasongo Pia ni Baba wa Msanii wa Camp Mula Afariki Dunia

Mwanamuziki wa bendi ya Orchestra, Kasongo wa Kanema ambaye ni mzaliwa wa Congo ambaye amekaa Kenya kwa miaka zaidi ya 30 amefariki akiwa nyumbani kwake Nairobi.

Bendi hiyo ilijipatia umaarufu kwenye miaka ya 1970 kwa nyimbo zilizotamba sana kama Shauri yako, Matata Sipendelei, Sina Kazi, Nyumbani ni Nyumbani na nyingine nyingi.

Mwanamuziki huyo pia ni baba wa msanii Shappaman ambaye ni miongoni mwa wasamii wanaounda kundi la Camp Mulla la Kenya.

Miaka mitatu iliyopita mwanamuziki huyo alifanya mahojiano na alisema kati ya wanakundi 13 wa bendi hiyo ni 4 tu ndio walikuwa hai. Hivyo baada ya yeye pia kutangulia mbele za haki wamebaki watatu tu.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey