VIDEO : Msanii Pam D afunguka Jinsi Alivyofutiwa Video Zake Youtube
MKALI anayekimbiza kwenye gemu la Bongo Fleva, Pamela Daffa ‘Pam D’ ametinga ndani ya Mjengo wa Global Group kutambulisho ujio wake mpya wa Kizunguzungu akiwa na Frank Ferdick ‘Foby’ huku akisimulia kuumizwa na watu waliomfutia nyimbo katika Mtandao wa Youtube.
Akisimulia Julai 3, 2019 mchana ndani ya Kipindi cha Bongo 255 kinachoruka hewani kupitia +255 Global Radio, Pam D alianza kwa kuwashukuru mashabiki kwa kusapoti kazi zake tangu ameingia kwenye muziki kwani amekuwa akipambana mwenyewe kwa kila kitu.
“Nawashukuru sana mashabiki wangu kwa kuwa pamoja nami lakini kuna kitu kinaniumza sana, kuna mtu aliingia katika akaunti yangu ya Youtube kipindi cha nyuma na kufuta nyimbo zangu mbili Popolipopo na Nimempata na ndiyo chanzo cha kuziweka kwa mpigo zote mbili,” alisimulia Pam D ambaye mwaka jana alitikisa na Ngoma ya Yeyo na Imepenya.
Kwa upande wa Foby ambaye aliambatana naye alimzungumzia Pam D jinsi alivyokutana naye na kumtaka kutengeneza wimbo huo wa pamoja wa Kizunguzungu.
“Pam D alinicheki na kuniambia kuna ngoma anataka nikae ambayo ni hii ya Kizunguzungu, nikamwambia mbona ngoma imeshakamilika unataka tu kunikalisha.
Nikawa najiuliza sana naweza kuwa na melody lakini mimi nabembeleza sana, akanilazimisha sana nikamwambia sawa tukaipika,” alisema Foby na kuongeza kuwa Pam D ni kati ya watu aliokuwa akiwakubali kabla ya kutoka kwenye gemu.
Pakua App ya +255 Global Radio ili Kusikiliza Vipindi vyetu, Bofya HAPA KUINSTALL APP
STORI: ANDREW CALOS, GPL