Willy Paul Amlilia Mwanamke Instagram Kisa Nandy
Msanii kutoka Kenya Willy Paul ambaye anatamba katika Ukanda huu wa Afrika Mashariki kwa Kuachia hits kali kama vile ‘Halelujah’, Njiwa Alizomshirikisha Msanii kutoka Bongo, Nandy amezua gumzo katika mitandao ya kijamii baada ya kutumia Ukurasa wake wa Instagram Kumlilia Msanii mwenzie ‘Alaine’ kutoka Jamaica.
Willy Paul na Alaine wamekuwa ni marafiki wa karibu sana hasa baada ya kutoa wimbo wa ‘I Do’ ambao ulifanya vizuri sana katika tasnia ya Muziki Afrika Mashariki. Kupitia Instagram yake Willy Paul ametoa siri kuwa hivi sasa yeye na Alaine sio marafiki tena na kuwa Alaine amemblock kitendo ambacho kimemuumiza sana, kwani alizoea kuona Likes na Comments za Alaine kwenye picha zake na hata akimpigia simu amekuwa hapokei na hajibu Meseji zake. Willy Paul ameandika
“Alaine, we were so good together dear, to be honest meeting you was the best thing ever coz it was like a dream come true.. when u see a man admitting to such, that’ means something big. I woke up today feeling some type of way, you use to like my pics and comment on them.. nowadays I call you and you dont pick.. you dont even reply to my messages.. tell me have I wronged you in anyway? No I dont think so, like I said, i had so much hope in this..” begged Willy Paul on Instagram.
Willy Paul amezidi kufunguka na kueleza kuwa hata mama yake mzazi amekuwa akimuuliza kuhusu Alaine na kuongeza kuwa hapaswi kumchukia kwa sababu ya Ukaribu wake na Nandy kwani Nandy ni rafiki yake tu wa kawaida.