Wasanii Hawa wa Gospel Bongo, Nyimbo Zao Lazima Ubarikiwe!
KIPINDI Bora cha mambo ya kiroho kinachoruka kila Jumapili kuanzia saa 12:00 hadi saa 3:00 asubuhi, SOUL FOOD kupitia +255 Global Radio kimezidi kukimbiza huku wasanii mbalimbali wa gospel nchini wakizidi kumiminika studio kutambulisha kazi zao kwa mashabiki wao na kushea mambo mbalimbali yanayohusu imani na kumcha Mungu.
Jana Jumapili, Oktoba 27, 2019 waimbaji watatu wa Gospel ambao ni Lily Max, Frida Rotson na Calvin Kangoye Mahende walitinga kwenye studio za +255 Global Radio zilizopo Sinza Mori jijini dar es Salaam kutambulisha kazi zao ambazo wamekuwa wakifanya kwa ajili ya kumtukuza Mungu na kuitangaza injili kupitia gospel.
Ndani ya SOUL FOOD, Lily ambaye ni mwimbaji wa nyimbo za kuabudu, alitambulisha albumu yake ya Live recording iitwayo ‘WEWE U MWEMA’, ambayo inatikisa sokoni.
Lily ambaye alikuwa akihudumu katika Kanisa la Calvary Assemblies of God lililo chini ya Apostle Maboya, mjini Morogoro, amesema kwa sasa amehamia rasmi jijini Dar es Salaam, na anatoa huduma katika Kanisa hilo hilo (Calvary) Branch ya Dar linayoongozwa na mke wa Maboya, lililopo Ubungo Maziwa.
Amesma sababu za kuhamia Dar ni kuusogeza mbele kazi zake za muziki wa injili na kufanya harakati zake za masuala ya sheria ambayo ni taaluma yake.
Kwa upande wake Frida, aliutambulisha wimbo wake uitwao Upengo wa Mungu, huku akitambulisha pia wimbo wake mwingine mpya ambao ameachia hivi karibuni uitwao SIWEZI BILA WEWE.
Naye Kangoye ambaye ni mwimbaji Chipukizi wa nyimbo za injili, alitambulisha wimbo wake mpya uitwao, YESU ANATAWALA.
Mbali na kutambulisha kazi zao, waimbaji hao pia walipata fursa ya kujadili kuhusu MAMOMBI YENYE MAJIBU ambapo kila mmoja alitoa moni yake kwa mtazamo wake na namna ambavyo vitabu vya dini vinaelekeza.