Mama ake Nicki Minaj kuja na wimbo wa Injili aliomshirikisha mwanae
Mama wa Nicki Minaj, Carol Maraj amefunguka kuwa atapenda kushirikiana na binti yake (Nicki Minaji) kwenye wimbo wa injili.
Hivi karibuni Mama yake Nicki Minaj amekuwa akikumbatia talanta yake ya uimbaji na kuanza kufanya kazi zake mwenyewe. Na hivi karibuni katika msimu wa joto, Carol Maraj aliachia wimbo wake uitwao “What Makes You.” Katika mahojiano mapya, Carol alifunguka kwamba angependa kushirikiana na binti yake, Nicki Minaj kwenye wimbo wa Injili.
Maraj aliliambia jarida la PEOPLE, kwamba anaamini pendo la Nicki kwenye muziki lilitokana na yeye, kwani yeye “aliimba wakati wote toka alipokuwa binti mdogo.
Toa Maoni Yako Hapa