‘Bright anaamini nimemroga’ – Elly Da Bway afunguka ukweli wote
MSANII na mtayarishaji wa muziki wa kizazi kipya Bongo Elly Da Bway amezungumzia tuhuma zilizokuwa zikimuandama kuwa amemroga msanii mwenzake Bright ambaye walikuwa wakifanya kazi ya sanaa pamoja
Kupitia mahojiano aliyoyafanya kwenye kipindi cha Bongo255 kinachorushwa na +255 Global Radio Msanii huyo aliweza kukanusha madai hayo kwa kusema; “Mimi sijamroga Bright ila kama anaamini nimemroga sawa sababu kurogwa ni kutokuwa na imani.” Alisema Elly.
Ni kweli mimi kwetu ni sumbawanga hivyo sishangai watu kuhisi hayo, Issue ilianzia kwenye kazi nilimuita tufanye video ya wimbo wangu niliomshirikisha lakini location hakutokea, tulimpigia simu toka asubuhi aje location hakupokea simu; na baadaye akapokea akasema mimi nipo njiani naenda kumuuguza Mama Morogoro, Kisha alikuja akasema turudie video….tukapanga kila kitu na hela ya nguo nimemtumia na nilianda kila kitu ilipofika siku yenyewe hakutokea simu, Hivyo nikaamua kuendelea mbele kushoot na watu wengine.” Alongeza Elly.
Hii inakuja baada ya Bright kudai Elly emekuwa akimroga na akaamua kumuondoa kwenye video aliyoshirikishwa na msanii huyo.