Picha: Uni Bash Carnival ya Global Radio ilivyotikisa chuo kikuu Dar es Salaam ‘UDSM’
NOVEMBA 29, 2019, ilikuwa siku ya kihistoria na kiburudani kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu CHA Dar es Salaam (UDSM), baada ya radio ya mtandaoni inayotamba kwa sasa nchini, +255 Global Radio kufika chuoni hapo kuzungumza na wanafunzi hao na kufanya Bonge la tamasha lililopewa jina la Uni Bash Carnival.
Timu nzima ya +255 Global Radio ambao ndio waandaji wa tamasha hilo ilijumuika na wanafunzi wa chuo hicho ikiwa na dhumuni la kuwaburudisha na kuwaelimisha kuhusu mabadiliko makubwa ya teknolojia ya habari na mawasiliano.
Katika Tamasha hilo lililofanyika kwenye viwanja vya chuo hicho huku kukiwa na burudani za kutosha kutoka kwa Ma DJs wakali, zawadi kemkem, wanafunzi hao pia walipewa elimu kuhusu namna ya upatikanaji wa matangazo ya moja kwa moja ya +255 Global Radio ambayo inatumia mfumo wa teknolojia ya mtandaoni kurusha matangazo yake.
Sambamba na hayo +255 Global Radio ilifanikiwa kunadi vipindi vyake vyote vinavyoruka redioni kwa wakati tofauti tofauti ndani ya saa 24 siku 7 za wiki.
Aidha katika tamasha hilo wanafunzi wa UDSM waliweza kufundishwa namna ya kusikiliza kupakua Aplikesheni ya redio kupitia simu zao za mkononi na kompyuta.
Baadae burudani kali ilishushwa na DJ’s mahiri kutoka +255 Global Radio wakiongozwa na Dj Super, Dj Big Daddy na Dj Obway, sambamba na utambulisho wa watangazji wote wa vipindi kutoka +255 Global Radio chini ya Meneja wao, Borry Mbaraka.