French Montana atangaza ujio wa Album yake mpya akiwa chumba cha wagonjwa
FRENCH Montana bado yupo hospitali akipokea matibabu lakini hiyo haijamzuia asifanye kazi zake, ametangaza tarehe ya kuiachia album yake mpya.
Mkali huyo ambaye yupo chini ya Epic Records ametuweka wazi kuwa album hiyo Montana itatoka Ijumaa hii (Disemba 6), tamko hilo amelitoa akiwa katika chumba cha wagonjwa ambapo bado anaendelea kupokea matibabu tangu November 21.
24/7 #Tunakusanua Kinachoendelea Kwenye Ulimwengu Wa Burudani | Kutusikiliza au kupakua app ya radio Bonyeza Hapa
Toa Maoni Yako Hapa