BASATA Wamfutia Usajili Dudubaya Kujihusisha Na Sanaa
Baraza la Sanaa la Taifa (@basata.tanzania) lamfutia rasmi usajili msanii Dudubaya baada ya kugoma kuitikia wito kutoka kwa Baraza hilo lililopewa jukumu la kusimamia kazi za sanaa nchini. Kupitia ukurasa wao katika mtandao wa kijamii Intagram BASATA wametoa taarifa hiyo kwa kusema…
KUMFUTIA USAJILI MSANII GODFREY TUMAINI a.k.a DUDUBAYA
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) ambalo ni msimamizi wa sekta ya Sanaa nchini limemfutia usajili msanii Godfrey Tumaini a.k.a Dudubaya kutokujihusisha na shughuli zozote za sanaa kuanzia leo tarehe 07/01/2020.
Baraza limechukua hatua hii baada ya msanii huyu kukiuka wito wa Baraza la Sanaa la Taifa ambao ulimtaka kufika BASATA kwa mujibu wa sheria na kanuni za Baraza, Msanii huyu aliitwa na Baraza kutokana na alichokizungumza kuhusiana na wasanii na sekta ya Sanaa kupitia Mitandao ya Kijamii kwa makusudi amekaidi wito wa Baraza.
Kwa mantiki hii BASATA halitavumilia wasanii wachache ambao wanataka kuigeuza sekta ya sanaa kwa kutumia lugha chafu na isiyo na staha mbele ya jami.
Baraza linatoa onyo, kwa Taasisi, Kampuni na mtu yeyote kutofanya kazi ya sanaa na msanii huyu.
Baraza linawakumbusha wasanil na wadau wote wa sanaa nchini kufanya kazi kwa weledi kwa kuzingatia sheria, kanuni, taratibu na miongozo inayosimamia sekta ya sanaa nchini pamoja na kuzingatia sheria za ndhi.
. “Sanaa ni kazi, tuikuze, tuilinde na kuithamini”