Sambaza

DJ Khaled Atoa Msaada wa ‘Mask’ 10,000

Mtayarishaji nguli wa muziki Dj Khaled ameamua kuwasaidia wale walioko mstari wa mbele kwenye vita hii ya kupambana na virusi vya Corona na sio wengine bali ni wafanyakazi wa afya.

DJ huyo alitangaza siku ya J’Nne (Machi 31) kuwa atashirikiana na wenzake wawili kutoa msaada wa vifaa muhimu kwa wafanyakazi wa afya. Watatu hao watatoa vifaa hivyo kwenye hospitali zilizopo Miami na New York.

Kutokana na janga la virusi vya corona kuwa kubwa, hospitali nyingi zimekuwa na upungufu wa vifaa vya kujikinga na wafanyakazi wa afya wamekuwa kwenye mazingira hatarishi hivyo msaada wa DJ Khaled na wenzake utasaidia kwa kiasi kikubwa.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey