Jay Z, Meek Mill Watoa Mask 100,000 Jela
Waanzilishi wa REFORM Alliance Jay Z, Meek Mill na wengine wametangaza kutoa msaada wa barakoa ila wamechagua sekta ya tofauti ambayo wengi hawakuitazama kama inapaswa kupata misaada ya kujikinga na virusi vya Corona, magereza.
Wasanii hao na wenzao wamechangia barakoa 50,000 kwenye gereza la Rikers Island Jijini New York ambapo kulikuwa na maambukizi 231 kwa wafungwa na 223 kwa wafanyakazi wa gereza hilo.
“Serikali na watu wanaosimamia haya magereza wanapaswa kuchukulia hili suala la gereza la Rikers kama onyo” alisema mwakilishi wa REFORM Alliance.
Hii ni mara ya pili Jay Z anahusika moja kwa moja kutoa msaada ambapo mapema wiki hii alitoa msaada mwingine ambao ulitoka kwenye kampuni anayomiliki kwa pamoja na msanii Rihanna.
Toa Maoni Yako Hapa