Sambaza

Simtamani Harmonize, Mume wa Mtu Hapana, Itokee Tu

Mwanadada aliyeonekana kwenye video mbili za Harmonize “Uno” na “Bedroom” Nicole Joy Berry ameweka wazi kuwa hamtamani Hermonize kwa namna yoyote ile sababu ameoa.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Online Tv aliulizwa na mtangazaji Tilda Mohit kama anatamani kuwa mwanamke wa Harmonize siku moja na akajibu kwa msisitizo “NO ameoa.”

Pia mwanadada huyo aliulizwa kuhusu kuhusishwa kutembea na wanaume walio kwenye ndoa na alisema “Siwezi kutembea na mwanaume wa mtu, labda itokee hapo baadaye mimi sio mkamilifu ila mpango huo sina.”

Mbali na hayo, Nicole ameweka wazi kuwa Video vixen huwa hawalipwi vizuri hivyo hana mpango wa kuwa video vixen wa msanii yeyote atakayetaka kufanya naye kazi kwa pesa. Msanii pekee anayeweza kufanya naye kazi ni yule ambaye wana urafiki au ukaribu wa namna yeyote au anamuheshimu ila sio msanii ambaye atakuja kwa gia ya mkwanja.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey