Sambaza

Waziri Afafanua Aina Tatu za Barakoa, Muda wa Kuzivaa

Kupitia mahojiano aliyofanya na kipindi maalumu cha @255globalradio ambacho pia kumerushwa LIVE kwenye You Tube chanel ya @globaltvonline Dkt. Faustine Ndugulile, Naibu Waziri wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii ametolea ufafanuzi aina za barakoa na namna zinavyopaswa kutumika.

“Kwa sasa hivi kitaalamu tuna aina tatu kubwa,” alisema Naibu Waziri huyo na kuongeza  “Kuna barakoa za N95, hizi ni za kiwango cha juu sana, kuna za upasuaji (zenye rangi mbili) na ya mwisho ni barakoa za nguo au kitambaa.”

Akitolea ufafanuzi wa namna za kutumia barakoa hizi, Dkt. Ndugulile alisema “Hizi za N95 ndizo zinazotumika na madaktari wetu wanaohangaika na wagonjwa, hizi tunasisitiza zitumike na madaktari au wanaohudumia mgonjwa na hizo za upasuaji (Surgical Mask) zitumike na wauguzi wengine ambao hawamuhudumii mgonjwa moja kwa moja na pia wananchi wa kawaida wanaweza kuzitumia pia.”

Akizungumzia barakoa za vitambaa amesema kuwa zinaweza kutumika japo bado kuna mkanganyiko juu ya aina hizo za vitambaa kwa sababu shirika la afya Marekani linasema kuwa zinaweza kutumika wakati shirika la afya la dunia (WHO) lenyewe linasema kila nchi ifanye tathmini ya kina kuhusu utumiaji wa barakoa za vitambaa au nguo.

Pia Naibu Waziri amesisitiza kuwa matumizi ya barakoa sio mbadala bali inapaswa iende sambamba na jitihada nyingine za kujikinga kama kunawa na kujiepusha na misongamano.

Mwisho amesisitiza kwa kusema “barakoa sio ya kuvaliwa kutwa nzima, haipaswi kuzidi masaa 4 mpaka 6 .”

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey