Mtoto wa Bob Marley ‘Ziggy Marley’ Azungumza Kuhusu Mazingira
Kijana wa kwanza wa nguli wa muziki wa Rege Bob Marley, David Nesta “Ziggy Marley” ametoa njia ambazo zinapaswa kufanywa ili kuepusha madhara zaidi kwa mazingira.
Yeye binafsi amenunua gari la umeme ili kuepusha kutumia mafuta ambayo yana mchango mkubwa kuharibu mazingira, na pia amepunguza matumizi ya vifaa vya plastiki.
Ziggy amesema “kuwafunza watu wa viwandani kutumia pesa zao vizuri ni moja ya hatua kubwa kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na viwnda.”
Pia aliongeza kuwa kusema “viwanda vinapokua, faida ndiyo inayowatawala zaidi kuliko afya, hiyo haipaswi kuwa hivyo wanapaswa kuzingatia afya za watu.”
Pia amesisitiza kuwa jukumu la kutunza mazingira sio la serikali pekee wala sio la wananchi pekee bali wanapaswa kufanya kazi kwa pamoja kuhakikisha wanaitunza dunia.