Aunt Ezekiel Afichua Siri Kutorudiana na Iyobo
Staa wa Bongo Aunt Ezekiel amesema zamani alijitahidi kumrudisha mzazi mwenziye walipokuwa wamegombana kwa ajili ya furaha ya mtoto wao Cookie lakini sasa hivi anaangalia furaha yake na ndio maana amekubali matokeo.
“Yaani kuna kitu kinaumiza sana, unajaribu mno kujishusha mpaka hatua ya mwisho lakini wapi, na hiyo ilikuwa kumpa furaha mtoto wangu huku ya kwangu ikiteketea, hiyo nimeikataa. Sasa furaha yangu kwanza na kama baba atazoea tu wengine watakaokuja,” alisema muigizaji huyo.
Aunt anasema anachokiamini ni kuwa mtoto wake anampenda sana baba yake kupita maelezo, lakini kwa sababu hakuwa tayari japo alijishusha vya kutosha ni bora tu maisha yaendelee.
Toa Maoni Yako Hapa