Mastaa Wakerwa na Tukio la Polisi Kumuua Mmarekani Mweusi
Huku kukiwa kuna maandamano ya kupinga ukatili kwa watu weusi nchini Marekani, jambo ambalo limeamshwa na kifo cha mwanaume mmoja aliyefahamika kwa jina la George Floyd ambaye aliuwawa na polisi kumuwekea goti kwenye koo na kupelekea kifo chake. Baadhi ya mastaa nchini humo na duniani kote wameonyesha wazi hisia zao za kukerwa na tukio hilo.
Naomi Campbell
Kipitia ukurasa wake wa instagram, mwanamitindo huyo aliandika “hili litaishia wapi?” huku akiwa ameweka picha iliyoambatana na maneno aliyoongea kijana huyo wakati akipigwa na polisi.
Justine Bieber
Mwanamuziki huyo naye hakuwa nyuma kuhakikisha kuwa anaungana na wote wanaopinga ukatili huo na kutumia ukurasa wake wa instagram wenye wafuasi milioni 137 kuweka video fupi na kuandika maneno “hili ni lazima liishe” akimaanisha ubaguzi na ukatili unapswa kuisha.
Cardi B
Rapa huyu alikwenda mbali zaidi kwa kuita kitendo kilichofanywa na polisi huyo ni kitendo cha kipuuzi na kisichopaswa kufumbiwa macho na kumalizia kwa maneno “Inatosha.”
Joe Biden
Mwanasiasa huyu ambaye ndiye aliyepewa dhamana na chama chake kugombea urais kwenye uchaguzi unaokuja naye hakukaa kimya kwenye jambo hili baada ya kuweka ujumbe kwenye ukurasa wake wa twitter na kuandika “George Floyd anastahili mazuri na familia yake inastahili kupata haki.”