50 Cent Awajibu Wanaosema Amemwagwa na Mpenzi Wake Kwa Video 1 Tu
Tetesi za kuvunjika kwa penzi la rapa 50 Cent na Cuban Link zilitambaa sana mtandaoni lakini 50 Cent amewajibu wote kwa video moja tu ambayo ameiweka kwenye mtandao wa Instagram.
Baada ya kuwa na mahusiano kwa mwaka mmoja, tetesi za kuachana kwa wawili hao zilikuwa kubwa mwezi huu ila wote wameweka picha aambazo zinaashiria kuwa bado wapo pamoja.
50 Cent aliweka video ikimuonyesha dada mmoja akiwa amening’inia kwenye gari ambalo linatembea na kutaani kuwa ni mpenzi wake Cuban Link jambo ambalo linafanya wengi kupigia jibu mstari kuwa lazima watakuwa wapo pamoja bado la sivyo asingekuwa huru kuweka utani huo.
Toa Maoni Yako Hapa