Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Baraka The Prince, amefunguka kwamba mara ya kwanza wakati anakuja jijini Dar es Salaam kipindi akitafuta njia ya kutoka kimuziki, alikuja kwa ndege tofauti na wasanii wengi ambao mara ya kwanza walikuja kwa basi.
Baraka amesema mama wa msanii mwenzake, Bob Junior, ndiye aliyeenda kumpokea uwanja wa ndege baada ya kuwasili jijini Dar es Salaam akitokea Mwanza.
Kauli hiyo ya Baraka imekuja baada ya msanii mwenzake, Tundaman kueleza kwamba yeye ndiye aliyempa nauli ya basi Baraka wakati anakuja mjini kwa mara ya kwanza jambo ambalo mwenyewe amelikanusha.