Harmonize Avunja ‘Mwiko’ wa WCB, Amfollow Alikiba
Tetesi za Msanii Harmonize kuondoka katika lebo ya WCB zimeendelea kutikisa katika mitandao ya kijamii hapa Bongo hasa baada ya Harmonize kufuta neno ‘Signed Under WCB Label’ kwenye Ukurasa wake wa Instagram.
Harmonize ameendelea kuwaaminisha watu kuwa huenda akaondoka au ameshaondoka WCB hasa baada ya kuendelea kufanya mabadiliko kwenye kurasa zake za Mitandao ya kijamii. Kitu kingine kilichowaaminisha watu ni kitendo chake cha kuamua ‘Kumfollow’ Alikiba kwenye akaunti yake ya Instagram kitendo ambacho hakuwahi kukifanya kwa muda wote akiwa WCB. Alikiba na Diamond Platnumz wamekuwa wapinzani wa kimuziki kwa muda mrefu na wasanii wote wa WCB hawajaifollow akaunti ya Alikiba isipokuwa Harmonize pekee ambaye ameamua kumfollow hivi karibuni.
Kitendo hicho kimetafsiriwa kama ‘Kuvunja Miiko’ ya WCB na kuwa moja kati ya ishara kuwa hayuko tena chini ya lebo hiyo.