Kim Kardashian Ametangaza Tarehe Ya Kuachiwa ‘Jesus Is King’ Ya Kanye West
Albamu mpya ya Kanye West Jesus Is King ilikuwa imepangwa kuachiwa rasmi jana (Septemba 27), hata hivyo albamu hiyo ilisogezwa mbele kwa sababu ambazo hazikujulikana mara moja. Kim Kardashian ambaye ni mke wake ameitangaza jumapili ya Septemba 29 kama siku ambayo albamu hiyo itaingia sokoni.
Kupitia Instagram stori, Kim ameandika kama Kanye anafanya listening party Chicago leo Jumamosi halafu New York kesho Jumapili, kinachosubiriwa ni mixing chache zilizobaki kuikamilisha albamu hiyo yenye nyimbo za dini.
Albamu mpya ya #KanyeWest #JesusIsKing ilikuwa imepangwa kuachiwa rasmi (Septemba 27), hata hivyo ilisogezwa mbele kwa sababu ambazo hazikujulikana mara moja. #KimKardashian ambaye ni mke wake ame|https://t.co/K2wPxLaPR4 pic.twitter.com/iXx0Nd7WVN
— 255 Global Radio (@255globalradio) September 28, 2019
Ujio wa albamu hii ulitangazwa rasmi mwezi August, ambapo mke wa Kanye, Kim Kardashian West ali-post picha yenye orodha ya nyimbo kumi na mbili zilizoambatana na tarehe 27 Septemba. Jana Septemba 28, Kim Kardashian amepost tracklist mpya yenye nyimbo kumi na moja ukiwemo New Body ambao Kanye ameripotiwa kuufanyia kazi kwa muda mrefu.
Have faith… pic.twitter.com/2HF4HiPQoq
— Kim Kardashian West (@KimKardashian) September 27, 2019
Mwaka mmoja kabla ya kutangaza ujio wa ‘Jesus Is King’, Kanye alitangaza angeachia ‘Yandhi’, Albamu ambayo ilighairishwa kwa kile ambacho Kanye alisema atatangaza tarehe ya kuiachia atakapokuwa ameikamilisha.
2,221 total views, 9 views today