Wini ajitapa kununua gari aina ya Harrier Lexus ‘Kama kuna mwanaume anayejiamini ajitokeze’
MSANII wa muziki wa Bongo Fleva Wini Tz, ambaye amesema kama kuna mwanaume yeyote anayejiamini na anasema amemnunulia gari ajitokeze amuone.
Wini Tz amesema hayo baada ya kuwepo na taarifa zinazosema gari analotumia aina ya “Harrier Lexus” amehongwa na mwanaume wala hajanunua kwa pesa zake mwenyewe.
View this post on Instagram
Eti ili pozi la picha tuliitaje?? #finestgirl #farmgirl #ADO click the link on my bio
“Mishe zangu ni kupambana kama mtoto wa kike, nasimama kama mimi bila kumtegemea mwanaume yeyote yule, kwa hiyo nilipambana kwa mihangaiko ambayo nimeifanya kama Wini, kupitia muziki wa “live band” na kilimo changu ndipo nilipo jibariki na kitu kama kile” amesema Wini Tz.
Aidha msanii huyo ameongeza kusema “Kwa hiyo kama kuna mwanaume ambaye anaamini yeye kanunua lile ndinga aje hapa au nyinyi mleteni yule mnaemjua nyinyi, wasichana tunaweza sio mpaka uwe na miaka 80 huko au 90 ndiyo ununue gari, sikuhizi vijana tunapambana tunatakiwa tubadilishe akili zetu” ameongeza.
Pia amesema hawezi kuwahukumu wanawake wanaotumia njia fupi ili kutengeneza maisha yao, wala hawezi kuwashauri wafanye vibaya, na hawezi kudhibiti nafsi za watu, kila mtu anayetamani kufanya vitu vyake afanye ila kwa njia iliyo salama.