Tanasha Akanusha Penzi Lake Na Diamond Kuwa Na Mgogoro
Tanasha Donna amedai kuwa penzi lake na mwanamuziki Diamond Platnumz liko imara na kuwaondoa hali wasiwasi waliodhani kuwa kuna uwezekeno wa penzi hilo kuvunjika.
Hali imekuja kutokana na kuibuka kwa tetesi kuwa Diamond yupo kwenye mahusiano ya siri na mwanamke mwingine ambaye mpaka sasa jina lake halijafahamika.
Kupitia Insta Story yake, Tanasha ameweka picha yake akiwa mithili anakiss na Diamond na kuandika: ‘Unbreakable’ akimaanisha kisichovunjika kwa maaana kwamba mapenzi yao hayavunjiki.
Tayari Tanasha amezaa mtoto mmoja na Diamond Platnumz anayejulikana kwa jina la Naseeb Jr.
Toa Maoni Yako Hapa