‘Katambuga’ Yawaka Rasmi Global Radio (Picha +Video)
Watangazaji wa kipindi cha Uswahilini cha Katambuga (Kijiwe Dobo) wakipokelewa na wafanyakazi wa Global Group jana Sinza-Mori jijini Dar es Salaam.
JANA Agosti 16, 2019, kulifanyika uzinduzi rasmi wa Kipindi cha Uswahilini cha Katambuga (Kijiwe Dobo) kinachoruka kila siku za Jumatatu hadi Ijumaa katika spika za +255 Global Radio.
Katambuga ni kipindi maalumu kinacholenga zaidi maisha ya Uswahilini, hasa ku?chua na kutatua matatizo na changamoto za jamii mbalimbali ambacho huruka kuanzia saa 12 jioni hadi saa 2 usiku chini ya watangazaji mahiri, Odo Aisha (Kubwa la Maninja), Zari Baby na Gaby Mtanzania (Sauti ya Mwanaume).
Uzinduzi huo ulihudhuriwa na mastaa mbalimbali akiwemo Mama Kanumba, Ben Selengo, Kiroboto OG ‘Mzee wa Matarumbeta’, akiwemo Mkurugenzi Mtendaji wa Global Group, Eric Shigongo na wafanyakazi wa makampuni hayo.
Mhariri Mtendaji wa Global Publishers, Saleh Ally, ndiye aliyeongoza shughuli hiyo ikiwemo sapraizi ya kuwapokea watangazaji wa hao wa Katambuga na kuongoza zoezi zima la ukataji keki lililoambatana na uzinduzi wa kipindi hicho.
“Tumeamua kufanya hiki kitu sisi kama uongozi tukishirikiana na hawa watangazaji wa Katambuga kwa kutambua uwezo na kazi yao kubwa wanayoifanya hasa ya kuisaidia jamii,” alisema Ally.
Akizungumza kwa niaba ya Katambuga,Odo Aisha alisema: “Tunaushukuru uongozi kwa kutambua uwezo wetu na kazi kubwa tunayofanya kwa kuwa tumekuwa sehemu ya kutatua matatizo ya jamii na tunaahidi kuongeza ubunifu zaidi.”
Naye Shigongo ambaye alizungumza mambo mengi yenye mafundisho, alisema: “Endeleeni kufanya hicho mnachokifanya na sisi kama uongozi tutawasaidia, msiogope kufanya jambo kwa hofu ya kushindwa huko mbele, jitumeni na muonyeshe vipaji vyenu ambavyo Mungu amewapa.”
Ili kusikiliza ‘live’ matangazo ya +255 Global Radio, tembelea tovuti ya https:// globalradio.co.tz/ au pakua App ya +255 Global Radio katika Play Store kwa kuandika 255 Global Radio.