Kanye West Ameshinda Kesi Inayohusisha Kustaafu Muziki
Takribani miezi minane imepita tangu uzuke ugomvi wa kisheria kati ya Kanye West na EMI,kampuni ambayo ni wasambazaji wa muziki wake. Taarifa zilizotufikia, Kanye na EMI wamefikia makubaliano na huenda ugomvi wao ukafika mwisho. Ripoti iliyotolewa inadai pande zote mbili zimekubaliana kuvunja mkataba wao ndani ya siku 90.
Mwezi Januari Kanye West alifunga mashitaka akitaka kujiengua kwenye kampuni hiyo ambayo amekuwa akifanya nayo kazi tangu mwaka 2004 alipoiachia albamu ya kwanza ‘College Dropout”. Kanye anadai mkataba wake na EMI unamzuia kustaafu muziki kitu ambacho hataki kukubaliana nacho. Bado haijatambulika kama Kanye West anajipanga kustaafu masuala ya muziki muda huu, lakini tunachokifahamu ni ujio wa Albamu yake ya nyimbo za dini “Jesus Is King” itakayoachiwa Septemba 27 mwaka huu.