Bobi Wine Amefanikiwa Kuwatoroka Polisi
Mwanamuziki ambaye ni Mwanasiasa pia, Robert Kyagulanyi maarufu Bobi Wine amefanikiwa kutoroka ulinzi mkali wa Polisi uliokuwa ukizingira nyumba yake huko Magere.
Inadaiwa kuwa kwa sasa Mbunge huyo wa Kyadondo Mashariki anaelekea kwenye Tamasha lake alilozuiwa kulifanya huko Busabala kwa kutumia Bodaboda.
Mapema leo asubuhi Polisi walizingira nyumba ya Bobi Wine ili kumzuia kushiriki katika Tamasha lake la muziki liitwalo ‘Osobola ku Independence’ kwa Kiingereza ‘Independent Day Music Concert’. Kwa mujibu wake Bobi Wine amedai kuwa Polisi walianza kuzingira nyumba yake na ukumbi wa tamasha hilo jana usiku huku akidai Polisi hao ndio walisema hawana uwezo wa kulinda watu huko Busabala.
Aidha, Msemaji wa Polisi, Fred Enanga ameeleza kuwa tamasha hilo haliwezi kufanyika kwa sababu Bobi Wine ameshindwa kutofautisha Siasa na Muziki
1,958 total views, 3 views today