Odemba Aliyoyapitia Kabla ya Kuwa Staa, Project Zake Mpya
Mwanamitindo maarufu duniani, Miriam Odemba (36) amefunguka kuhusu maisha aliyopitia kabla ya kuanza harakati zake za sanaa ya mitindo hadi kuwa maarufu.
Akipiga stori na Global Radio leo Jumanne, Oktoba 29, 2019, aliyekuwa ameambatana na matroni wake, Bi. Mary Vonne Paul ambaye pia ni Balozi wa Kuheshimiwa nchini Shelisheli (Seychelles).
“Nimeishi katika mazingira magumu sana namshukuru Mungu hapa nilipofika aliongeza kusema. Nimekua nikishirikana na Mama yangu kwenye kazi zangu, amenisaidia mambo mngi sana, mama ndo kila kitu kwangu,” amesema Odemba.
Miriam amesema amerejea Tanzania akitokea Ufaransa ambapo ana projekti yake ya kusaka vipaji kupitia tasnia ya mitindo (Model Talent Search) ambapo jana alizindua rasmi jijini Dar es Salaam.
Odemba ameendelea kueleza kuwa kwa sasa tayari ana vijana watatu ambao anafanya nao kazi ili kukuza vipaji vyao kazi.
Ameongeza pia kwamba kwa sasa ana taasisi yake inayofahamika kama Odemba Foundation inayoendelea kujikita zaidi kwenye masuala ya kijamii hasa akina mama na watoto.
Mrimbwende huyo ambaye pia aliwahi kuwa Miss Temeke mwaka 1997, amesema anachokifanya kwa sasa ni kulipa fadhila kupitia mafanikio aliyopata kwa jamii inayomzunguka.
Odemba ambaye mwaka 1998 aliingia kwenye kinyang’anyiro cha Miss East Africa, kupitia African Reflection Foundation Miriam ameteuliwa kuwa Balozi wa Maji ambapo mradi huo wa visima umefanyika wilayani Mukuranga mkoani Pwani, na tayari visima 128 vishachimbwa kwa ajili ya matumizi ya wananchi.
Full video ya interview znima na ODEMBA utaipata kupistia GLOBAL TV Online.
Matukio katika Picha.