UCHAMBUZI: DIWANI MDOGO ZAIDI TZ NI ‘KICHWA’
Zamani kulikuwa na dhana tofauti ya kuwa huwezi kuwa kiongozi bora kama ukiwa na umri mdogo na uhalisia sio hivyo, Namshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amekuja kufanya mapinduzi kwa vijana, kwanza yeye mwenyewe ameonyesha wazi kuwaamini vijana na kuwapa fursa. Hii ni kauli toka kwa Diwani wa kata ya Kijichi Elias Mtarawanje alipokuwa akizungumza leo katika kipindi cha 255FrontPage kutoka @255globalradio ..
“Kuwa kijana ni kitu kingine na kufanya kazi bora ni kitu kingine, kuwa kijana haikufanyi kuwa bora zaidi; bali ubora wako utaonekana kulingana na utendaji wako, usikivu wako, na nidhamu yako na jinsi gani unafanya kulingana na utaratibu. Vijana huu ni wakati wetu tunahitaji kuonesha jamii kuwa tunaweza kufanya na kuhudumia jamii yetu.” Alisema Mtarawanje.
“Sababu sisi tuna nguvu, tuna uwezo wa kwenda umbali mrefu. Tuwaonyeshe dhahiri wazee waliotuamini kwa kipidi hiki na uaminifu wao kwetu una maana; na hayo yote yanawezekana kwa vijana.” Aliongeza.
Kuaminika kwetu inatakiwa sasa ile imani tulipewa tuionyeshe kwa vitendo.