Sababu Zilizomsukuma Hayati Benjamin Mkapa Kugombea Urais
Pengine unaweza ukawa haufahamu kwanini Hayati Benjamin Mkapa aliamua kuchukua fomu ya kugombea Urais.
Simulizi kutoka katika kitabu chake, ‘My Life, My Purpose’ anaweka wazi kuwa alisukumwa na mambo makubwa manne.
Kwanza, alitaka kurekebisha na kurejesha uhusiano chanya kati ya chama na serikali yake na vyama vya ushirika ambao ulikuwa umefifia.
Pili, alitaka kuimarisha uhusiano na vyama vya wafanyakazi ambao walikuwa wanatishia kugoma kwa mara ya kwanza.
Tatu, ilikuwa kurekebisha mahusiano mabaya na wahisani kutokana na kushamiri kwa rushwa.
Nne, alitaka kurudisha uhusiano na mashirika ya fedha ya kimataifa, amabao walikuwa wamekataa kuanzisha miradi mipya na mwisho aliwapima waliokuwa wamechukua fomu akaona atajilaaumu hapo baadae kama naye hatagombea.